Nuru International

Nuru International ina dhamira ya kukomesha umaskini uliokithiri katika maeneo ya vijijini. Huanzisha miradi ya maendeleo katika jamii inayosimamiwa na wenyeji, kama vile Nuru Kenya na Nuru Ethiopia, ili kupata mipango inayolenga zaidi masilahi ya jamii kwa jumla – katika Kilimo, Ujumuishaji wa Kifedha, Huduma za Afya na Elimu – ili kushirikisha jamii yote katika juhudi za kukomesha umaskini katika vizazi mbalimbali.

Kiasi cha Utendaji

Wastani

Sekta

Kimataifa, Masuala ya Nchi za Kigeni

Malengo

Changisha pesa

Hamasisha

Ongeza tija na uboreshe shughuli

Bidhaa

Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida

Aliyepiga Picha

Picha za Nuru International katika tovuti hii zilitolewa na Nuru International.

Tovuti

https://www.nuruinternational.org/

Changamoto

Nuru imefanya kila iwezalo kuondoa gharama za huduma ili fedha zinazochangishwa ziende kuelimisha viongozi wa maeneo mahususi kupitia zana na ujuzi ili kuongoza jumuiya zao kuondoka kwenye umaskini uliokithiri. Kama shughuli pepe, Nuru hutegemea ofisi za nyumbani na nafasi za kufanya kazi pamoja badala ya ofisi kuu Marekani, ambayo huisaidia kuwekeza zaidi kwenye jumuiya zake za washirika. Wafanyakazi wake wanahudumu maeneo 11 yenye saa tofauti, kumaanisha wanategemea zana za kidijitali kushirikiana.

Hadithi

Shirika la Nuru limenufaika kutokana na zana za Google Workspace. “Katika kampuni yoyote, watu hutumia teknolojia kwa viwango tofauti,” alisema Kim Do, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Mikakati. “Google Workspace imetusaidia sana kwa sababu ni suluhu ya pamoja, kumaanisha kuwa tunafunza timu yetu kutumia kifurushi kimoja cha zana kwa njia nyingi zaidi.”

Nuru inaweza kutumia Ramani za Google inaposhirikiana kati ya walio Marekani na walio kwenye eneo la tukio. Licha ya kuwa mbali sana, ofisi zilizo Marekani zinaweza kupokea picha ya kinachotendeka na inaweza kusaidia kuhakikisha wafanyakazi wake wako salama kwa kuhakikisha kuwa wanatii mipaka ya maeneo husika na kuzuia kuchochea vurugu ambayo inaweza kutokea iwapo hawakufahamu hivyo. Hata wamejumuisha ramani katika kufunza wafanyakazi wapya. “Nuru hutumia Photo Sphere na Taswira ya Mtaa kusaidia wafanyakazi wapya kukagua kwanza miradi yetu nchini Kenya na Ethiopia hata kabla hawajafika,” alisema Brian von Kraus, Mshauri wa Mikakati ya Usalama. “Pia, kuwa na uwezo wa kubuni ramani zilizowekewa mapendeleo huwezesha wafanyakazi wetu wa eneo husika kuona kiwango cha athari na idadi ya wakulima waliosaidiwa.”

Pia wametumia YouTube kufikia hadhira pana. “Video ni muhimu katika mawasiliano yetu kwa sababu ni mbinu yetu ya msingi ya kuunganisha wahisani Marekani na wakulima tunaohudumia katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara. Inapendeza kuona wafadhili wetu wanavyovutiwa na dhamira na maono yetu baada ya kuona kazi tunayofanya Kenya na Ethiopia kupitia filamu,” alisema Kim Do, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kimkakati. “YouTube hutupa uwezo wa kuchapisha video zetu mpya kwa njia bora na inayofaa kwa kuwa wafadhili wetu wana shughuli nyingi popote walipo. Pia, tunapenda sana jinsi YouTube wanavyoturuhusu kuweka mapendeleo kwenye ukurasa wetu, hivyo kupanua hali ya shirika letu.”

“Video ni muhimu katika mawasiliano yetu kwa sababu ni mbinu yetu ya msingi ya kuunganisha wahisani Marekani na wakulima tunaohudumia katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.”

Kim Do, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kimkakati.

Athari

Hali ya kufanya kazi katika muda halisi kupitia zana za kushirikiana kwenye Google Workspace imesaidia shirika la Nuru kufanya shughuli zake za kila siku vizuri zaidi na kwa ufanisi kwenye maeneo 11 yanayotumia saa tofauti za eneo. Wametumia Viendelezi vya Google kama vile “Rekebisha Chaguomsingi za Tukio” ili kupunguza barua pepe zisizo muhimu wanapopanga mikutano. Huwa wanatumia viungo vya Hifadhi ya Google badala ya kuambatisha faili ili kila mfanyakazi apakue — hatua ambayo inasaidia haswa katika maeneo yasiyo na muunganisho thabiti wa Intaneti. Kufanya kazi katika maeneo ya vijijini ambako umeme hukatika mara kwa mara, kipimo kidogo cha data na uwezo mdogo wa kufikia muuzaji rejareja na kurekebisha kompyuta kunamaanisha kuwa ni muhimu kudhibiti maarifa. Shirika la Nuru limeweza kupanga mbinu za kudhibiti maarifa ili kukabili vikwazo hivi.

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.