Maswali Maarufu Yanayoulizwa Sana

Tumia ukurasa huu ili upate majibu ya maswali yanayoulizwa sana kuhusu mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.

Je, hupati unachotafuta?

Angalia Kituo chetu cha Usaidizi

  • Mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida na bidhaa zake unapatikana katika kila nchi ulimwenguni?

    Kwa sasa, mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida unapatikana katika zaidi ya nchi 65 (angalia upatikanaji wa nchi hapa). Tafadhali rejelea chati hii ili uone bidhaa zinazopatikana katika nchi uliko.
  • Masharti ya kujiunga na mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida ni gani?

    Ili kutimiza masharti ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, ni lazima mashirika yawe mashirika ya kutoa misaada yasiyo ya faida yenye hadhi nzuri katika nchi yaliko na yathibitishwe kuwa shirika lisilo la faida na mshirika wa uthibitishaji wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida Percent. Angalia masharti ya kujiunga ya nchi husika hapa.
  • Sina uwezo wa kufikia akaunti ya mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida katika shirika langu. Ninaweza kuomba uwezo wa kufikia kwa njia gani?

    Iwapo huna uwezo wa kufikia akaunti ya uanachama wa mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida katika shirika lako, unaweza kuomba uwezo wa kuifikia kwa kufuata hatua zilizobainishwa hapa.
  • Percent ni nini na ina jukumu gani katika mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida?

    Shirika la Percent linashirikiana na kampuni kama vile Google ili kuunganisha mashirika yasiyo ya faida duniani kote kwenye zana za teknolojia, nyenzo na maarifa wanayohitaji ili kuhudumia jumuiya zao.

    Shirika la Percent huangalia maelezo ya kisheria na ya mradi yanayohusiana na shirika lako ili kuthibitisha hadhi yake kama shirika lililosajiliwa kisheria na la faida kwa jamii, lisilo la faida na kuwa shirika lisilo la serikali. Pata maelezo zaidi kuhusu Percent.

  • Mimi ni shirika la afya, taasisi ya serikali au shule isiyo ya faida. Je, ninatimiza masharti ya kujiunga na mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida?

    Hapana. Kwa wakati huu, shirika lako halijatimiza masharti ya kujiunga na mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida. Iwapo wewe ni shule, kituo cha kutunza watoto, taasisi ya elimu au chuo kikuu, angalia mpango wa Google for Education.
  • Mimi ni shirika la Marekani lililobuniwa chini ya kifungu cha 501(c)(3) lenye hadhi ya shirika la kutoa misaada kupitia mpango wa kundi la kutotozwa ushuru unaotolewa na shirika kuu. Je, ninatimiza masharti ya kujiunga na mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida?

    Iwapo shirika lako lina hadhi ya shirika la kutoa msaada kupitia mpango wa kutotozwa ushuru wa vikundi unaotolewa na shirika kuu, huenda bado linatimiza masharti ya kujiunga na mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida. Ni lazima liwe tawi tofauti linalolindwa kupitia mpango wa kutotozwa ushuru wa vikundi na ni lazima Google iweze kuthibitisha kupitia hati za umma, kuwa shirika lako liko chini ya shirika kuu lililothibitishwa kupitia mpango wa kundi la kutotozwa ushuru.

    Ili uanze, ingia katika akaunti ya mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida na uweke nambari ya EIN ya shirika lako kuu. Iwapo kuna mashirika mengine tanzu yanayotumia EIN sawa ya mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, utaombwa utume ombi jipya. Ukifanya hivyo, hakikisha kuwa umebofya 'Anza kutuma ombi jipya'. Usiombe umiliki wa shirika lolote tanzu ambalo hulifahamu.

    Pata maelezo zaidi kuhusu mpango wa kundi la kutotozwa ushuru.
  • Je, shirika langu linalofadhiliwa kutoa ushuru linatimiza masharti ya kujiunga na mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida?

    Hapana, mashirika yanayofadhiliwa kutoa ushuru hayatimizi masharti ya kujiunga na mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.