Saraka za Washirika wa Bidhaa Walioidhinishwa

Soma ukurasa huu ili upate washirika waliothibitishwa na wenye ujuzi wa kukupa usaidizi kuhusu jinsi ya kutumia bidhaa za mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida.

Google Workspace

Anza kutumia Google Workspace ipasavyo kwa kupata usaidizi kutoka kwa Mshirika wa Wingu la Google ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Google Workspace. Iwe unatafuta usaidizi wa kuhamia kwenye huduma au usaidizi kamili kwa mkakati wako wa Google Workspace, Washirika wa Google Workspace wa Wingu la Google wataharakisha mradi wako na kuboresha matokeo yako.

Ruzuku za Google Ad

Jumuiya ya Wataalamu Waliothibitishwa wa Ruzuku za Google Ads imebuniwa ili kuboresha hali ya matumizi ya Ruzuku za Google Ad kwa wataalamu na Wanaopokea Ruzuku pia. Jumuiya hii inatambua mtandao wa mawakala, washauri na waelimishaji wanaochunguza mashirika yasiyo ya faida duniani kote na kuwaunganisha Wanaopokea Ruzuku na wataalamu wanaopendekezwa kupitia Saraka ya Jumuiya yetu.

YouTube

Geuza ari yako kuwa vitendo. Gundua nyenzo za YouTube na utafute kampuni zilizoidhinishwa kama Stadi katika Maswala ya YouTube, ambazo zinaweza kukusaidia ulete mabadiliko zaidi.

Jukwaa la Ramani

Anza kutumia Jukwaa la Ramani za Google vizuri kupitia usaidizi kutoka kwa Mshirika wa Wingu la Google ambaye ni mtaalamu wa Jukwaa la Ramani za Google.