Royal National Lifeboat Institution

RNLI, Royal National Lifeboat Institution, ni shirika la kutoa misaada ambalo huokoa maisha baharini. Tangu mwaka wa 1824, wafanyikazi na wapiga mbizi wa kitaalamu wa boti za uokoaji wameokoa angalau maisha ya watu 140,000 baharini kupitia michango ya uhisani.

Kiasi cha Utendaji

Wastani

Sekta

Umma, Manufaa ya Jamii

Malengo

Andikisha, funza na uwasiliane na watu wanaojitolea

Hamasisha

Pata wafadhili

Bidhaa

Ruzuku za Matangazo kutoka Google

Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida

Aliyepiga Picha

Nigel Millard/RNLI

Tovuti

https://rnli.org/

Changamoto

RNLI huokoa kwa wastani maisha ya watu 24 kwa siku. Inatoa huduma ya uokoaji na utafutaji kupitia boti za uokoaji mchana na usiku katika Uingereza na Ayalandi na huduma ya kimsimu ya wapiga mbizi wa kitaalamu. Ili kudumisha shughuli kama hii, RNLI hutegemea michango ya wafadhili wake — hali inayomaanisha kuwa uhamasishaji wa shirika hili ni muhimu zaidi.

Hadithi

RNLI hutumia zana za Google ili kuwapa wafadhili waliopo hali bora zaidi ya utumiaji – na kuwavutia wafadhili watarajiwa.

Shirika hili la misaada lina zaidi ya vituo 230 vya boti za uokoaji katika Uingereza na Ayalandi – na kila boti ya uokoaji ina kamera ambayo hurekodi shughuli zote za uokoaji. Video ya matukio ya moja kwa moja huchapishwa kwenye YouTube, ili kuwaonyesha wafadhili waliopo umuhimu wa misaada yao. Iwe ni mashua inayoyumbishwa katika mawimbi makali au mbwa aliyeokolewa majini na kurudishiwa mmiliki wake, maudhui haya halisi yanayoweza kushirikiwa pia hutangaza kazi ya shirika hili lisilo la faida kwa hadhira ya watu wenye umri mdogo. Kituo cha YouTube cha RNLI kwa wastani hutazamwa mara 75,000 kwa mwezi na kina watu 10,000 wanaokifuatilia.

Tangu mwaka wa 2005, RNLI imekuwa ikitumia Google Ads na Ruzuku za Matangazo ili kulenga wafadhili wapya – wafadhali bora kwa wakati unaofaa. Miaka kumi baadaye, wakati RNLI ilikuwa ikiangaziwa kwenye makala maarufu ya hali halisi ya BBC, mpango wa Ruzuku za Matangazo ulitumiwa kusaidia katika uhamasishaji kwa njia bora zaidi. Kupitia maudhui yanayofaa na ulengaji bora wa hadhira, ilipata idadi kubwa ya michango na watu waliotembelea tovuti.

RNLI imetumia Google Analytics kwa muda mrefu ili kuchanganua idadi ya wanaotembelea tovuti na mienendo ya watumiaji. Tangu mwaka wa 2014, takwimu hizi zimetumika katika mikakati ya kwanza ya maudhui pana ya shirika. Katika RNLI, watu hawaangalii tu ripoti – wanachukua hatua kuzihusu. Wanachukua hatua ili kuhakikisha kuwa maudhui ya mtandaoni yanafaa hadhira na kuwa tovuti zinavutia vitendo ambavyo shirika linahitaji.

“Hatua ya kutumia zana ambazo Google hutoa imetuwezesha kugundua njia mpya za kutangaza shirika letu la kutoa misaada na kazi inayofanywa na wafanyakazi wetu wa kujitolea.”

Nigel Saxon, Msimamizi wa Emedia, RNLI

Athari

Kama shirika lisilo la faida ambalo hupokea 92% ya mapato yake kutokana na michango, RNLI ina uwezo wa kuendelea kuokoa maisha baharini kila siku huku ikipigwa jeki na mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida ambao huongeza kutambulika kwake na kiasi cha michango inayotolewa.

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.