Fikia wafadhili zaidi mtandaoni ukitumia Ruzuku za Matangazo kutoka Google

Vutia wafadhili, tangaza shirika lako na uandikishe watu wanaojitolea ukitumia ufadhili wa matangazo kwenye huduma ya Tafuta na Google.

Ruzuku za Matangazo hukupa uwezo wa kufikia USD $10,000 za ufadhili wa matangazo kila mwezi kwa matangazo ya maandishi.

Manufaa

Jinsi Ruzuku za Matangazo kutoka Google hufanya kazi

Utapokea USD $10,000 za ufadhili wa matangazo kutoka Google kila mwezi ili utunge matangazo yanayotokana na maandishi na upate uwezo wa kufikia zana za kukusaidia kuanzisha kampeni bora ambazo zinaweza kuonyeshwa kwenye huduma ya Tafuta na Google watu wanapotafuta maelezo yanayohusiana na shirika lako lisilo la faida.

Gundua jinsi Ruzuku za Matangazo kutoka Google husaidia mashirika yasiyo ya faida kufikia wahisani zaidi na kupunguza vizuizi vya kutoa michango.

Zana nyingine za kukusaidia ufikie wafadhili zaidi mtandaoni

Mbali na Ruzuku za Matangazo kutoka Google, bidhaa nyingine zinazotolewa kupitia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida zinaweza pia kukusaidia utangaze shirika lako na uchangishe pesa.

Tuma ombi la kufungua akaunti ya Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Baada ya kuthibitisha kuwa shirika lako limetimiza masharti, utaweza kuweka bidhaa za Google zinazotimiza mahitaji yako kikamilifu.

Je, una maswali au ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kutumia Ruzuku za Matangazo kutoka Google?

Baada ya shirika lako lisilo la faida kuthibitishwa na umejisajili kwenye Ruzuku za Matangazo, angalia nyenzo zetu na Maswali Yanayoulizwa Sana ili upate manufaa zaidi ya mpango.