Special Olympics World Games

Olimpiki Maalumu hutoa mafunzo ya michezo mwaka mzima na huandaa mashindano ya riadha kwa watoto na watu wazima wenye matatizo ya akili. Kupitia kazi yao, wanariadha wanaoshiriki hupata fursa ya kufanya mazoezi ya mwili, kuonyesha ujasiri na kuonyesha vipawa vyao kwa jumuiya ya ulimwengu.

Kiasi cha Utendaji

Wastani

Sekta

Huduma za Jamii

Malengo

Hamasisha

Malengo Kushirikisha hadhira

Pata watu wanaofuatilia shirika lako

Tathmini utendaji wa tovuti yako

Vutia watu wanaotembelea tovuti yako

Bidhaa

Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Ruzuku za Matangazo kutoka Google

Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida

Aliyepiga Picha

Olimpiki Maalum

Tovuti

https://www.specialolympics.org/

Changamoto

Wakati wa Michezo ya Ulimwengu mwaka wa 2015 mjini Los Angeles, wanariadha 6,500 kutoka nchi 165 walishiriki katika michezo 25 tofauti, wakionyesha maana halisi ya ujasiri, furaha na ukakamavu.

Ili kuzindua tukio hili kubwa, ilikuwa lazima kupanga watu 30,000 waliojitolea, watazamaji 500,000 na makumi ya mamilioni ya dola katika michango.

Simulizi

Ili kufanikisha Michezo ya Dunia ya 2015, shirika la Special Olympics lilitumia Google Workspace ili kuwapanga waliojitolea. Pia, lilitumia Ruzuku za Matangazo kuwashirikisha watazamaji mtandaoni na kutumia huduma ya Google Analytics ili kufahamu vyema hadhira yao lengwa.

“Dhamira yetu ya uhamasishaji unaosababisha kukubalika na kujumuishwa inamaanisha kuvutia watazamaji zaidi iwezekanavyo kupitia hadithi hizi maarufu. Google iliweza kutusaidia si tu kujua hadhira yetu lakini pia kupata hadhira ulimwenguni kote ili kuweza kusambaza ujumbe huo.”

Patrick McClenahan, Rais na Afisa Mkuu Mtendaji (CEO), 2015 Special Olympics World Games

Athari

Kampeni yao ya Ruzuku za Matangazo ilivutia asilimia 44 ya watumiaji wapya katika tovuti ya Olimpiki Maalumu na kushawishi nusu ya idadi hiyo kusajili.

Pia, Google Analytics iliwapa ufahamu kuhusu utendaji wa jumla wa tovuti na kuwaruhusu kupima kiasi na vyanzo vya kushirikisha walivyokuwa wakipokea.

Pia uwezo wa kufikia Studio ya YouTube jijini Los Angeles uliwasaidia kutunga maudhui ya video kwa kutumia bajeti ndogo, hatua iliyoendeleza uhamasishaji zaidi kuhusu malengo yao.

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.