Jane Goodall Institute

Jane Goodall Institute inaendeleza ufahamu na ulinzi wa sokwe wakuu na makazi yao kupitia msingi uliowekwa na Dkt. Jane Goodall, mwanzilishi wake, ili kuhimiza hatua za kibinafsi za watu wa umri wote zinazonuia kusaidia wanyama, watu wengine na kulinda ulimwengu tunakoishi.

Kiasi cha Utendaji

Kubwa

Sekta

Wanyama na Mazingira

Malengo

Changisha pesa

Hamasisha

Onyesha data kwenye ramani

Bidhaa

Aliyepiga Picha

Jane Goodall Institute

Tovuti

https://www.janegoodall.org

Changamoto

Lengo la Jane Goodall Institute ni kuhifadhi sokwe wakuu wa Kiafrika na makazi yao, kwa kuzingatia zaidi sokwemtu. Ili kutekeleza shughuli kwa ufanisi, miradi ya utunzaji inahitaji data na sayansi bora zaidi inayopatikana ili kubuni, kutekeleza, kupima na kufuatilia ufanisi wa vitendo vya utunzaji. Ni lazima pia ihusishe wadau kwa njia za uwazi na za kushirikisha — kuanzia kwa jamii za eneo husika hadi kwa mamlaka za serikali.

Hadithi

Mwaka wa 2006, Jane Goodall Institute (JGI) ilianza kushiriki taarifa za kila siku mtandaoni ambazo zilitoa taswira ya utafiti wa nyanjani kuhusu sokwemtu na ukaguzi endelevu wa mpango wa utafiti ulioanzishwa na Jane Goodall mwaka wa 1960.

Kwa kutumia zana za Google Earth katika kazi zake, imeweza kurekodi, kuchanganua na kushiriki maelezo kuhusu uharibifu wa misitu na jamii za eneo husika, wawakilishi wa serikali na wafadhili watarajiwa. Zana hizi za kuchakata na kuonyesha data zinashughulikia mambo zaidi ya data ili kutoa msingi ambako JGI inaweza kuonyesha kwa njia dhahiri makazi yanayoangamia na athari za umaskini, ikiwa ni pamoja na uharibifu wa misitu na changamoto za ukulima.

“Maelezo ambayo wachunguzi wa misitu wanakusanya si muhimu kwa wakazi wa kijiji pekee. Yanachangia katika juhudi za kimataifa za kuchunguza misitu na rasimali za asili kote duniani.”

Dkt. Lilian Pintea, Naibu Rais wa Sayansi ya Utunzaji, JGI

Athari

Kufuatia hamu na azma ya uhamasishaji wa awali ambao JGI ilifanya ya mtandaoni, imekuwa ikitumia Mtambo wa Google Earth, Open Data Kit (ODK), simu mahiri, kompyuta kibao na teknolojia ya wingu tangu mwaka wa 2009 kuziwezesha jamii za karibu ili kusimamia na kuchunguza misitu yao kwa njia bora zaidi.

Imetumia zana hizi kudhibiti matumizi ya ardhi na hifadhi za misitu katika magharibi mwa Tanzania, ili kuchunguza idadi ya viumbe hai katika eneo na kaboni katika misitu ya tropiki kavu na misitu ya Miombo na kubuni uwezekano wa kusambaza sokwemtu kwenye Mbuga za Kitaifa za Wanyama nchini Tanzania.

Vile vile, JGI imetengeneza programu ya Forest Watcher ambayo inarahisisha shughuli ya kupakua, kutambua, kuthibitisha na kuripoti kuhusu matukio ya uharibifu wa misitu na imebuni kozi ya mtandaoni kwa ajili ya mpango wake wa shughuli za vijana kwa kutumia programu ya Google ya Coursebuilder ambayo hutumia mpango wa Ramani Zangu na zana nyingine za Google za kuonyesha maeneo ili kufanikisha juhudi za utunzaji.

Nchini Uganda na Tanzania, JGI inatumia ODK na kompyuta kibao za Android ili kufanya uchunguzi wa kina kuhusu orodha na data ya wamiliki binafsi wa misitu ya kibinafsi na misitu ya vijijini ili kuchangia juhudi za kujitayarisha kwa nchi kwenye mpango wa REDD.

Kwa kushirikiana na Woods Hole Research Center na usaidizi wa Serikali ya Norwe, JGI imekuwa ikitumia teknolojia ya Mtambo wa Google Earth ili kufunza wafanyakazi nchini Tanzania wa kuchunguza idadi ya viumbe hai na kiasi cha kaboni katika misitu ya tropiki kavu na misitu ya Miombo.

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.