Direct Relief

Lengo la Direct Relief ni kuboresha afya na maisha ya watu walioathiriwa na umaskini au hali za dharura kwa kutoa nyenzo muhimu za matibabu zinazohitajika. Mipango yao ya kutoa misaada inalenga hali na mahitaji mahususi ya waathiriwa wa majanga ya kiasili au yanayosababishwa na binadamu.

Kiasi cha Utendaji

Kubwa

Sekta

Huduma za Jamii

Malengo

Hamasisha

Malengo Kushirikisha hadhira

Pata wafadhili

Bidhaa

Ruzuku za Matangazo kutoka Google

Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida

Aliyepiga Picha

Imepigwa na Direct Relief

Tovuti

https://www.directrelief.org

Changamoto

Kwa miaka kadhaa sasa, Forbes imelitaja shirika la Direct Relief kuwa miongoni mwa mashirika machache teule yaliyopewa ukadiriaji wa 100% katika ufanisi wa kuchangisha pesa. Direct Relief hujitahidi kufanikisha shughuli zake lakini inakabiliwa na changamoto inayokabili mashirika mengi yasiyo ya faida. Je, watu huwapata vipi? Kama shirika lisilo la serikali ambalo linategemea tu michango ya uhisani ya kibinafsi, linaweza kuimarisha vipi michango likiwa na rasilimali chache? Linaweza kufaulu vipi wakati matumizi yake ni madogo zaidi ikilinganishwa na mashirika mengine?

Hadithi

Direct Relief inaamini kuwa mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida unajibu maswali haya na zaidi kupitia zana nyingi za Google.

Shirika huendeleza utangazaji kupitia mtambo wa kutafuta kupitia Ruzuku za Matangazo na kupata maarifa kuhusu wafadhili na kufuatilia jinsi wanavyotumia tovuti kwa kutumia Google Analytics. Watu wanaweza kutambua kwa kuona juhudu za kimataifa za Direct Relief kwenye tovuti yake kwa kutumia Ramani za Google. Mguso wa hisia na wa kielimu unaotokana na video kwenye kituo cha YouTube cha shirika hufanya ujumbe wake uvutie na hupanua ufahamu kuhusu shirika.

“Kufikia tarehe 1 Januari — mwisho wa kilele cha msimu wa kutoa misaada ya mwisho wa mwaka — matokeo yalionyesha ongezeko la 44% la mwaka hadi mwaka katika idadi ya michango ya mtandaoni na ongezeko la 40% katika jumla ya dola zilizochangishwa mtandaoni.”
Athari

Katika miaka mitatu ya kwanza ya kupewa ruzuku ya Google mwaka 2003, Direct Relief ilikuwa na ongezeko la 6,000% la watu wanaotembelea tovuti yake. Lakini Google iliona uwezekano mkubwa zaidi, na ilifanya kazi bega kwa bega na Direct Relief ili kuboresha utendaji mtandaoni.

Mpango mpya wa masoko ulihusisha aina nane za kampeni katika utafutaji wa kulipishwa na utangazaji upya, na takriban matangazo 150 mapya ya maandishi ambayo yalianza kuonyeshwa wiki ya kwanza ya mwezi Desemba. Kufikia tarehe 1 Januari — mwisho wa kilele cha msimu wa kutoa misaada ya mwisho wa mwaka — matokeo yalionyesha ongezeko la 44% la mwaka hadi mwaka katika idadi ya michango ya mtandaoni na ongezeko la 40% katika jumla ya dola zilizochangishwa mtandaoni.

Jumla ya waliotembelea tovuti iliongezeka kwa 84%. Matangazo mapya ya masoko yalisababisha ongezeko la 2% katika watu wanaotembelea tovuti. Hoja za utafutaji zinazolipiwa na biashara (zile zinazojumuisha aina tofauti ya “Direct Relief”) zilishawishi asilimia 26 ya waliotembelea tovuti.

Ili kupiga hatua, Direct Relief inapanga kuendelea kuboresha kampeni zake za Ruzuku za Matangazo, pamoja na kushirikisha hadhira yake kwa upana zaidi kupitia hadithi zenye mafunzo na zinazoshawishi zaidi kwenye YouTube.

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.