Chief Almir na kabila la Surui la Amazon

Tangu mwaka wa 1968, wakati ambapo sisi, Wapaita, tulianza kutangamana “rasmi” na watu weupe, uhusiano na watu wasio Wahindi umesababisha mabadiliko makubwa katika jamii yetu. Hata hivyo, mabadiliko haya hayajakomesha moyo wetu wa ushujaa, ambao ulitupa ari ya kutetea eneo letu litambuliwe na lijumuishwe.

Kiasi cha Utendaji

Ndogo

Sekta

Wanyama na Mazingira

Malengo

Changisha pesa

Hamasisha

Onyesha data kwenye ramani

Bidhaa

Aliyepiga Picha

Chief Almir na kabila la Surui la Amazon

Tovuti

https://www.paiter.org

Katika historia yetu ya hivi majuzi, ardhi yetu imehatarishwa kabisa na mpango wa vurugu wa Polonoroeste, ufisadi na kutowajibika kwa mashirika ya serikali na shughuli haramu kwenye mazingira kama vile uchimbaji wa madini na upasuaji wa mbao.

Sisi, Wapaita, pamoja na watu walio kwenye misitu, tumejitolea kudumisha utamaduni na mazingira yetu ya kuishi.

Changamoto

Watu wa kabila la Surui wanaoishi katika Amazon nchini Brazil walitangamana na watu kutoka nje kwa mara ya kwanza mwaka wa 1969, hali iliyowaletea utamaduni wa kisasa na matatizo yote yanayotokana nayo. Baada ya miaka kadhaa, uhusiano huu uliendelezwa kwenye mazingira yao, yalipoanza kuhatarishwa kupitia uharibifu wa misitu na wakataji haramu wa miti.

Hadithi

Chief Almir alipogundua Google Earth kwa mara ya kwanza baada ya kutembelea mgahawa wa intaneti, chifu huyo alielewa mara moja uwezo wake wa kutunza turathi na tamaduni za watu wake. Alialika Google itoe mafunzo kwa jamii yake kwa kurekodi hadithi za wazee wa mitaa. Wanajamii wa kabila la Surui walijifunza kurekodi video za YouTube, kuweka lebo za kijiografia kwenye maudhui na kuyapakia kwenye "ramani ya utamaduni" kwenye Google Earth ili kushiriki historia yao ya kipekee na njia ya maisha na watu duniani kote.

Kwa wakati huu, uharibifu wa misitu ya kuleta mvua nchini Brazil una athari mbaya kwa wenyeji na uchumi wa eneo hilo na pia unaharibu uanuai wa viumbe na kuchangia katika utoaji wa gesi joto. Kwa sababu hizi, Cheif Almir anaamini kuwa tatizo la ukataji haramu wa miti katika eneo la kabila la Surui linaathiri kila mtu duniani na anatumia uwezo wa Google Earth kueneza habari.

Mwaka wa 2009, Google ilitembelea tena watu wa kabila la Surui na kuwafunza jinsi ya kutumia simu za mkononi na Open Data Kit ili kurekodi matukio ya ukataji haramu wa miti. Wanajamii wanaweza kurekodi video na kupiga picha zinazotambuliwa na GPS ili wazipakie mara moja kwenye zana za Google za kuchakata na kuonyesha data, kwa hivyo, wanaokata miti bila kibali siku hizi wanaweza kutambuliwa kwa urahisi; mtu yeyote aliye mahali popote anaweza kujionea athari za kazi yao.

“Tangu Google itoe zana za mafunzo kwa watu wa kabila la Surui na wenyeji wengine, nchi yetu imeonekana zaidi. Maelezo yote yanaangazia uvamizi wa ardhi yetu ... na kuwapa watu wetu wajibu wa kulinda mustakabali wao wenyewe.”

Chief Almir, San Francisco Chronicle

Athari

Sasa, watu wa kabila la Surui wanatumia Open Data Kit kufuatilia hisa ya kaboni ya msitu wao ili kufanya biashara katika soko la kaboni, hali ambayo itawaruhusu kudumisha mustakabali bora wa eneo lao.

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.