Fundación Todo Mejora

Shirika la Todo Mejora linajitahidi kuhakikisha masilahi ya vijana wanaojitambulisha na usagaji, ushoga, usenge na ugeuzaji wa jinsia (LGBT) kupitia mipango ya kuzuia kujiua na uchokozi unaolenga jumuiya ya LGBT.

Kiasi cha Utendaji

Ndogo

Sekta

Huduma za Jamii

Malengo

Shirikiana kwa ufanisi zaidi

Wasiliana na wahisani

Bidhaa

Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Ruzuku za Matangazo kutoka Google

Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida

Tovuti

https://www.todomejora.org

Changamoto

Chile ni mojawapo ya nchi zenye visa vingi zaidi vya vijana kujiua na vurugu shuleni katika Amerika Kusini. Pia, imeorodheshwa kuwa nchi ya pili kati ya nchi zilizo na asilimia kubwa ya kuongezeka kwa matukio ya kujiua katika Shirika la Maendeleo na Ushirikiano wa Kiuchumi (OECD)1. Data ya kitaifa inaonyesha kuwa iwapo hatua hazitachukuliwa, ndani ya miaka minne ijayo, kijana mmoja atajiua karibu kila siku2. Utafiti uliofanywa na UNICEF, Wizara za Maendeleo ya Jamii na Elimu na Todo Mejora unaashiria kuwa unyanyasaji kwa misingi ya mwelekeo wa kingono na utambulisho wa jinsia na kujieleza (SOGIE) huenea sana wakati wa kubalehe nyumbani, shuleni na kwenye jamii3. Katika matukio mengi, maneno ya hofu yanayohusiana na LGBT husikika kutoka kwa wafanyakazi wa shule, na hata wazazi wanapoarifiwa, hatua hazichukuliwi na wasimamizi wala wazazi4. Todo Mejora hujizatiti kubuni fursa ambako watoto na vijana waliobalehe watajihisi kuwa wanathaminiwa na kusaidiwa bila masharti katika matukio ya ubaguzi, kukataliwa kwenye familia na uchokozi wa maneno ya hofu yanayohusiana na LGBT.

Ili kubuni mazingira salama, Todo Mejora hutumia teknolojia kuboresha michakato yake. Timu hii ilijua kuwa ilihitaji kubuni kitovu kikuu cha habari ili kutengeneza kumbukumbu ya kitaasisi na kuhifadhi historia yake (hati, picha, video, anwani n.k.). Hatua hii ilihitaji kabati nyingi za kawaida za kuweka faili - Todo Mejora ilinuia kukuza ushirikiano, hivyo kuruhusu ufanisi na utendaji bora.

Jinsi yalivyo mashirika mengi yasiyo ya faida, Todo Mejora pia ililenga njia mpya za kufikia hadhira yake lengwa: Watoto na vijana wa LGBT wanaotafuta ushauri na usaidizi. Kwa kufanya hivyo, ilitumai kuhamasisha watu wengi kuhusu shirika nchini Chile. Kufikia hadhira pana ilikuwa muhimu hasa kwa kuwavutia wanaojitolea na wafadhili zaidi, hasa kupitia njia za dijitali.

Simulizi

Ili kuongeza uwezekano wa kufikia hadhira ya vijana wa LGBT, Todo Mejora iliamua kutumia Ruzuku za Matangazo kutoka Google. Lilitumai kuwa tangazo litatoa ujumbe wa tumaini na usaidizi, na pia kupata uwezo wa kufikia nyenzo za ziada. Kwa mfano, iwapo mtumiaji aliyefadhaika angetafuta “mawazo ya kujiua,” kwenye Google, angeona tangazo kutoka Todo Mejora, linalotoa ujumbe wa tumaini na hatua bora kuliko kujiua. Shirika pia lilichanganua hoja za utafutaji kama vile : "Ninataka kujiua", "Ninahitaji kuwasiliana na nani ninapotaka kujiua?", "Ni wapi ninaweza kumpeleka msichana wangu aliyejaribu kujiua?", "Nisaidie, ninataka kufa". Ingawa huu ulikuwa mchakato wenye hisia nyingi, timu hiyo ilijifunza jinsi ilivyo muhimu kuwasiliana na watumiaji ambao huenda wanatafuta usaidizi wakati wanapitia hali ngumu.

Shirika la Todo Mejora lilianza pia kutumia Google Workspace ili kuendesha shughuli zake kwa kutumia hifadhi ya GB 30 kwa kila mtumiaji na idadi isiyo na kikomo ya akaunti za watumiaji ili kuleta timu yake pamoja. Sasa, timu hiyo hutekeleza kazi zote za kila siku kwenye Gmail, Hifadhi na Kalenda za Google.

Kwa kutambua jinsi ujumbe unaoonekana ulivyo muhimu kwa vijana, Todo Mejora pia ilianza kutumia YouTube ili kushiriki masimulizi ya kibinafsi ambayo yangehamasisha jumuiya ya vijana wa LGBT nchini Chile. Timu hutumia matangazo yenye mwito wa kuchukua hatua yaliyowekelewa juu ya video zake ili kusaidia kutangaza dhamira na kufanikisha malengo makuu, kama vile kupokea misaada.

“Kilichotushangaza zaidi ni kuwa hatua hiyo ilifanya kazi! Ilipendeza sana kuona kile ambacho watu walikuwa wakitumia Google.com kutafuta kama vile: ‘Ninataka kujiua’, ‘Niwasiliane na nani ninapotaka kujiua?’, ‘Ninaweza kumpeleka wapi msichana wangu aliyejaribu kujiua?’, ‘Nisaidie, ninataka kufa’. Hali hii ilifichua mengi na machungu, lakini ilituhimiza kuimarisha kazi yetu na kutunga matangazo kutumia Ruzuku za Matangazo kutoka Google ili kutoa usaidizi kwa wale wanaouhitaji.”

Julio C. Dantas, Mwanzilishi wa Todo Mejora

Athari

Siku moja, msichana mwenye umri wa miaka 19 aliwasiliana na shirika la Todo Mejora kupitia vituo vya usaidizi na akasema: "Nilipofadhaika, nilitafuta jinsi ya kujiua kwenye Google. Shirika lenu, ’Todo Mejora,’ (inayomaanisha ‘Itakuwa bora’) liliibuka kwenye matokeo yangu ya utafutaji. Ilinifanya nitabasamu na ikanikumbusha umuhimu wa kuendelea kuishi.” Katika utafutaji wa kawaida kwenye Google, angechukua hatua nyingine. Lakini badala yake, alipata usaidizi kwa kuongea na wataalamu wetu kupitia kituo cha usaidizi. Siku hiyo tuliokoa maisha, kwa usaidizi wa Ruzuku za Matangazo kutoka Google!

Ujumbe huu wenye matumaini husaidia vijana wa LGBT kukabili hali ngumu na kupata matumaini. Tangu ianze ushirikiano wake na mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, Todo Mejora imeshuhudia mabadiliko dhahiri katika takwimu zake pia. Timu ilipata ongezeko la asilimia 20 kwenye idadi ya waliotembelea tovuti kupitia huduma ya Tafuta na Google kuanzia mwaka wa 2015 hadi 2016. Katika mwaka wa 2015, asilimia 55 ya waliotembelea tovuti walitumia mitandao ya jamii, ikilinganishwa na asilimia 28.6 kutoka huduma ya Tafuta na Google. Katika mwaka wa 2016, zilibadilishana nafasi na mitandao ya jamii ilielekeza asilimia 33.12 ya wageni, huku waliotembelea kupitia Utafutaji wakiwa asilimia 49.59.

Ongezeko hili kutokana na Ruzuku za Matangazo limefanya Todo Mejora kupanua vituo vyake vya usaidizi. Mwaka huu, shirika hilo lisilo la faida liliongeza saa za usaidizi kupitia simu kutoka saa 2 hadi 7 kwa wiki na linajitahidi kufikisha hadi saa 30 kwa wiki mwaka ujao.

Kwa sasa, shirika la Todo Mejora hutekeleza kazi zake zote za kila siku kwa kutumia Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida. Kazi zote huhifadhiwa kwenye Hifadhi ya Google na timu imegundua kuwa haihitaji kutegemea huduma au bidhaa nyingine kuhifadhi. Hali hii huwasaidia kuweka na kufikia hati zote kwa urahisi miongoni mwao. Kwa jumla, hatua hii imekuwa muhimu kwa kusaidia timu hiyo kukuza na kuendeleza kazi yake.

Todo Mejora imetumia zana za mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kukuza na kuimarisha shirika lake, kwa hivyo inaweza kulenga kuokoa maisha ya vijana wa LGBT kote katika Amerika Kusini.

1OECD (2016). Low Performing Students: Why They Fall Behind and How To Help Them Succeed. PISA. Chapisho la OECD. Paris
2 Ministerio de Salud de Chile (2013). Situación Actual del Suicidio Adolescente en Chile, con perspectiva de Género [Current Situation of Adolescent Suicide in Chile, with a gender perspective]. Programa Nacional de Salud Integral de Adolescentes y Jóvenes. Chile.
3 Fundación Todo Mejora (2016). Encuesta Nacional de Clima Escolar. Experiencias de Violencia e inseguridad Escolar de Estudiantes Lesbianas, Gays, Bisexuales y Trans [National School Climate Survey. Experiences of Violence and School Insecurity of Lesbian, Gay, Bisexual and Transgender Students]. Fundación Todo Mejora. Chile.
4Berger, Christian (2015). Bullying homofóbico en Chile: Investigación y Acción [Homophobic bullying in Chile: Investigation and Action]. Fundación Todo Mejora. Chile.

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.