Crime Victims Treatment Center

Crime Victims Treatment Center ni shirika lisilo la faida lililojitolea kusaidia watu kupona kutokana na uhalifu wa vurugu.

Kiasi cha Utendaji

Ndogo

Sekta

Huduma za Jamii

Malengo

Changisha pesa

Hamasisha

Imarisha usalama na faragha kwenye barua pepe

Wasiliana na ushirikiane kwa njia bora zaidi

Bidhaa

Google Workspace kwa Mashirika Yasiyo ya Faida

Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida

Aliyepiga Picha

Crime Victims Treatment Center

Tovuti

https://www.cvtcnyc.org

Tunaheshimu kwamba hali ya kupona hutokana na njia nyingi na tunatambua umuhimu wa mtazamo jumuishi. Crime Victims Treatment Center hutoa huduma nyingi za matibabu bila malipo kwa mtu yeyote aliyeathiriwa na vurugu. Tumejitolea kutetea waathiriwa, kushirikiana na washirika katika taaluma nyingi na kutoa mafunzo kwa wanaofanya kazi na waathiriwa. Tumejitolea kubadilisha kanuni za kitamaduni zinazohusu vurugu na kukuza haki ya kijamii kupitia sheria endelevu na uhamasishaji wa jumuiya.

Changamoto

Crime Victims Treatment Center inahitaji kusimamia na kuwasiliana na mtandao mkubwa wa wanaojitolea ili kuendeleza dhamira yake. Pia inahitaji njia ya kuhifadhi anwani za mawasiliano na mawasiliano ya barua pepe ya wagonjwa wake kwa usalama. Hatimaye, timu yake inahitaji mfumo thabiti wa waandishi wa ruzuku ili kushirikiana kwa urahisi kutoa mapendekezo mapya.

Hadithi

Crime Victims Treatment Center hutumia zana za Google kuwatibu wanafamilia na wanandoa wanaoathiriwa kupitia vurugu ya, unyanyasaji wa kingono, unyanyasaji wa kingono kwa watoto na aina nyingine za vurugu na uhalifu. Shirika hili hutumia mfumo wa kielektroniki ili kusimamia wanaojitolea kupitia Fomu za Google, kushirikiana katika maombi ya ruzuku kwa kutumia Hati za Google na kuhifadhi barua pepe zote za matukio ya malalamiko yanayotimiza masharti ya HIPAA kwenye Google Workspace. Shirika la Crime Victims Treatment Center hutumia pia Hangouts na YouTube kuendeleza kazi na dhamira yake kwa hadhira pana.

“Kuwekeza kwa teknolojia si chaguo tulilokuwa nalo. Mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida umetusaidia kuwekeza bila kujali gharama wala kutumia pesa ambazo hatuna kwa mambo ambayo tunahitaji sana.”

Christopher Bromson, Mkurugenzi Msaidizi

Athari

Kwa kutumia Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, Crime Victims Treatment Center huhifadhi maelezo nyeti kwa usalama na yakiwa yamepangwa, na pia kurahisisha mchakato usajili wa wanaojitolea. Kupitia matangazo ya YouTube, Crime Victims Treatment Center ilichangisha zaidi ya $40,000 kutokana na utangazaji wa 2014 wa tukio lao la manufaa la Broadway Unlocked. Kwa pamoja, huduma hizi tofauti hufanya iwe rahisi kwa Crime Victims Treatment Center kuendelea kuleta mabadiliko.

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.