Charity: Water

Watu milioni 663 duniani wanaishi bila maji safi. Katika Charity: Water, dhamira yetu ni kubadilisha hali hiyo kwa kuleta maji safi na salama ya kunywa kwa watu katika nchi zinazoendelea. Shirika linafanya kazi na washirika wake katika nchi za kigeni na limekamilisha zaidi ya miradi 21,000 ya maji na kufanya zaidi ya watu milioni 6.4 waweze kupata maji, huduma za usafi wa mwili na kudumisha mazingira safi.

Kiasi cha Utendaji

Kubwa

Sekta

Umma, Manufaa ya Jamii

Malengo

Changisha pesa

Hamasisha

Vutia watu wanaotembelea tovuti yako

Bidhaa

Ruzuku za Matangazo kutoka Google

Mpango wa YouTube wa Mashirika Yasiyo ya Faida

Aliyepiga Picha

Charity: Water

Tovuti

https://donate.charitywater.org/donate/home

Changamoto

Ili kusaidia kuleta maji safi na salama ya kunywa kwa kila mtu duniani, shirika la Charity: Water lilitaka kushirikiana kwa dhati na wahisani ili kuchangisha fedha, kuhamasisha watu wengi na kufikia wafadhili wapya kwa kuboresha upatikanaji wake mtandaoni.

Hadithi

charity: water ilidhamiria kupanua upatikanaji wake mtandaoni kwa kutumia zana zinazopatikana bila malipo kupitia Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida. Zana shirikishi, changanuzi, za jamii na za uboreshaji husaidia kuwaelimisha wafadhili watarajiwa huku zikitoa ushahidi unaoonekana kwa wahisani wake kuhusu jinsi michango yao inavyoleta mabadiliko ya moja kwa moja.

Kwa kutumia Ramani za Google, Charity: Water huunganisha wafadhili na kazi za ufadhili wao – baada ya kutoa mchango, wafadhili hutumiwa seti ya nambari na picha za GPS ambapo wanaweza kufuatilia michango yao na kuona mabadiliko inayoleta.

YouTube imeruhusu watu waliohusika na mradi wa maji kuweka kumbukumbu ya hatua zake kwa kutoa mfumo kwa wafanyakazi wa Charity: Water kutuma ujumbe wa kuwashukuru wafadhili au kurekodi video kwenye eneo la kazi ili kuelezea hadithi za binafsi ya jinsi visima vipya vya maji vilitoa maji salama na safi ya kunywa.

charity:water pia hutumia Ruzuku za Google Ad kusaidia kuboresha matokeo ya utafutaji yanayolipiwa na yasiyolipiwa ili kuanzisha kampeni kama ile iliyowahimiza watu kuwaomba marafiki zao na jamii kuchangia charity: water badala ya kutoa zawadi za kawaida za kuadhimisha siku ya kuzaliwa.

Dhamira yetu ni kuleta maji safi na salama ya kunywa kwa kila mtu duniani na kwa usaidizi wa Google, tunakaribia kufanikiwa kila siku.

Tyler Riewer, kiongozi wa maudhui ya kibiashara

Athari

“Katika mwaka mmoja, mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida ulisaidia kupata ongezeko la asilimia 350 la watu waliotembelea tovuti, ongezeko la asilimia 300 la jumla ya watu waliotembelea tovuti na ongezeko la asilimia 333 kwa waliotazama video.” alisema Tyler Riewer, kiongozi wa maudhui ya kibiashara, Charity: Water

Tangu timu ianze kutumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida, shughuli zao za mtandaoni zimeimarika kwa haraka. Shirika pia lilibuni jumuiya ya wahisani wenye ari kupitia video za YouTube zilizotoa ujumbe wa shukrani kwa watu mahususi, uwezo wa Ramani za Google na pia kupitia matangazo yanayotegemea utafutaji na mitandao jamii.

Na katika mwaka wa 2015, Charity: Water ulizindua kampeni yake ya kila mwaka ya kuchangisha mnamo Septemba. Ilikuwa na mada #NothingIsCrazy, ambayo iliwahimiza watu wajitolee kwa njia isiyo ya kawaida katika kuchanga pesa za kuleta maji safi. Kupitia usaidizi wa zana za Google, kampeni ilihamasisha karibu wachangishaji binafsi 1,900 na wakachanga dola milioni 1.8, ambazo zilileta maji safi kwa zaidi ya watu 60,000 katika nchi zinazoendelea. Google Analytics ilisaidia timu kuelewa washiriki, kubainisha asilimia ya walioshawishika na chati ya iliyoonyesha mara ambazo video ya tangazo la kampeni ilitazamwa.

Kwa sasa, Charity: Water inatumia uwezo wa kushawishi wa zana za Google kufikia hadhira mpya na kuwahimiza kuwekeza katika mazingira ambako kila mtu ana maji safi kwa kujiunga na mpango wa kuchangisha wa kila mwezi wa shirika hilo, The Spring.

Gundua jinsi mashirika mengine yanatumia mpango wa Google kwa Mashirika Yasiyo ya Faida kuleta mabadiliko.