Masharti muhimu

  1. Maelezo ya kibinafsi
  2. Akaunti ya Google
  3. Kidakuzi
  4. Kitambulishi kisichojulikana
  5. Anwani ya IP
  6. Kumbukumbu za seva
  7. Maelezo nyeti ya kibinafsi
  8. Maelezo yasiyotambulisha kibinafsi
  9. Lebo ya Pixeli

Maelezo ya kibinafsi

Haya ni maelezo unayoyatoa kwetu ambayo yanakutambulisha kibinafsi, kama vile jina lako, anwani ya barua pepe au maelezo ya utozaji, au data nyingine ambayo inaweza kuunganishwa kwa maelezo kama haya na Google.

Akaunti ya Google

Unaweza kufikia baadhi ya huduma zetu kwa kufunguaAkaunti ya Google na kutupatia maelezo yako kadhaa ya kibinafsi (kwa kawaida ni jina lako, anwani ya barua pepe na nenosiri). Maelezo haya ya akaunti yatatumiwa kukuthibitisha unapofikia huduma za Google na kulinda akaunti yako isifikiwe na watu ambao hujawaidhinisha. Unaweza kuhariri au kufunga akaunti yako wakati wowote kupitia mipangilio yako ya Akaunti ya Google.

Kidakuzi ni faili ndogo iliyo na msururu wa herufi inayotumwa kwa kompyuta yako unapotembelea tovuti fulani. Unapotembelea tovuti hiyo tena, kidakuzi huruhusu tovuti hiyo itambue kivinjari chako. Vidakuzi vinaweza kuhifadhi mapendeleo ya mtumiaji na maelezo mengine. Unaweza kuweka kivinjari chako upya ili kisikubalie vidakuzi vyote au kuonyesha kidakuzi kinapotumwa. Hata hivyo, vipengee vingine vya tovuti au huduma huneda visifanye kazi vizuri bila vidakuzi.

Kitambulishi kisichojulikana

Kitambulishi kisichojulikana ni msururu wa herufi bila utaratibu maalum zinazotumiwa kwa lengo sawa kama vidakuzi kwenye mifumo ya uendeshaji programu, pamoja na vifaa vya simu ya mkononi, ambapo teknolojia ya vidakuzi haipatikani.

Anwani ya IP

Kila kompyuta iliyounganishwa kwa Wavuti hupewa nambari ya kipekee inayojulikana kama Anwani ya Itifaki Wavuti (IP). Kwa sababu nambari hizi hutolewa kisehemu kulingana na nchi, anwani ya IP inaweza kutumiwa kutambua nchi ambamo kompyuta fulani imeunganishwa kwa Wavuti.

Kumbukumbu za seva

Kama tovuti mingi, seva zetu hurekodi maombi ya ukurasa yanayofanywa unapotembelea tovuti zetu kiotomatiki. “Kumbukumbu za seva” kwa kawaida hujumuisha ombi lako la wavuti, anwani ya IP, aina ya kivinjari, lugha ya kivinjari, tarehe na wakati wa ombi lako na moja au zaidi ya vidakuzi ambavyo vinaweza kutambulisha kivinjari chako kipekee.

Huu ni mfano wa kumbukumbu ambapo utafutaji ni wa “magari”, ikifuatiwa na sehemu zake:

123.45.67.89 - 25/Mar/2003 10:15:32 -
http://www.google.com/search?q=cars -
Firefox 1.0.7; Windows NT 5.1 - 740674ce2123e969

Maelezo nyeti ya kibinafsi

Hii ni aina ya maelezo ya kibinafsi inayohusiana na habari za siri za afya, asili ya rangi au kabila, imani ya kisiasa au dini au mwelekeo wa jinsia.

Maelezo yasiyotambulisha kibinafsi

Haya ni maelezo yanayorekodiwa kuhusu watumiaji ili yasionyeshe au kurejelea tena mtumiaji binafsi anayetambulika.

Lebo ya Pixeli

Lebo ya pixeli ni aina ya teknologia inayowekwa kwenye tovuti au katika kiini cha barua pepe kwa lengo la kufuata shughuli kwenye tovuti, au barua pepe zinapofunguliwa au kufikiwa, na hutumiwa pamoja na vidakuzi kwa kawaida.