Mfumo wa Kujisimamia

Ilibadilishwa mwisho tarehe: 1 Novemba 2012

Kama ilivyoelezewa katika cheti chetu cha Safe Harbor, tunatii Mfumo wa Safe Harbor wa Marekani na Muungano wa Ulaya na Mfumo wa Safe Harbor wa Marekani na Uswizi kama ilivyoelezwa na Idara ya Biashara ya Marekani kuhusiana na ukusanyaji, matumizi na uwekaji wa maelezo ya kibinafsi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya na Uswizi. Google imethibitisha ya kwamba inafuata Kanuni za Faragha za Safe Harbor kuhusu arifa, chaguo, uhamishaji, usalama, uthabiti, upatikanaji na utekelezaji wa data. Ili kujifunza zaidi kuhusu mpango wa Safe Harbor, na kuangalia cheti cha Google, tafadhali tembelea tovuti ya Safe Harbor.

Google ni mwanachama wa Network Advertising Initiative (NAI), ushirika wa makampuni ambayo yamejitolea kukuza sera za kuwajibika katika matangazo ya kibiashara kote kwenye Intaneti. Kwa kutumia zana iliyobuniwa na NAI, unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu makampuni mengine yanayotoa matangazo na kujiondoa kwenye matumizi yao ya vidakuzi kwenye tovuti ya NAI.

Google pia hufuata Kanuni za Shirika la Utangazaji la Uingereza kuhusu Desturi Bora za Kutangaza kulingana na tabia za mtandaoni, Mwongozo wa Australia kuhusu Desturi Bora za Kutangaza kulingana na tabia za mtandaoni na Mfumo wa Ulaya wa IAB kwa wa kutangaza kulingana na tabia za mtandaoni.