Hapa Google, tunafahamu vyema imani watumiaji wetu waliyo nayo kwetu, na jukumu letu kulinda faragha yao. Tunaamini uwazi na chaguo ni nguzo ya faragha. Ili kukusaidia kufanya uamuzi kuhusu faragha yako kwa kufahamika, tunajitahidi kukujulisha ni maelezo yapi tunayakusanya unapotumia bidhaa na huduma zetu na jinsi tunavyotumia maelezo hayo ili kuboresha huduma yako. Pia tunajitahidi, inapowezekana, kukupa chaguo za maana kuhusu maelezo unayoyatoa kwa Google na kwa wengine. Tunakuhimiza utazame video zetu, soma sera yetu ya faragha na urejeleea Vituo vyetu vya Msaada ili kujua zaidi kuhusu faragha katika Google.
Tunahifadhi data hii kwa sababu kadhaa. Ya muhimu zaidi, tunahifadhi data kuboresha matokeo yetu ya utafutaji na kudumisha usalama wa mifumo yetu. Kuchanganua kumbukumbu ya data husaidia wahandisi wetu kuboresha utafutaji wako na kuleta huduma zenye manufaa na za ubunifu. Chukua mfano wa Kikakuga Tahajia cha Google. Programu ya Google ya kukagua tahajia huangalia hoja ya mtumiaji kiotomatiki na kukagua kama mtumiaji anatumia maendelezo ya kawaida ya neno hilo. Tukipiga hesabu kuwa mtumiaji atapata matokeo bora zaidi kwa maendelezo mbadala, tutauliza “Ulimaanisha: (maendelezo ya kawaida)?” Ili kutoa huduma hii, tunachunguza data katika kumbukumbu yetu. Data ya kumbukumbu hutusaidia kuboresha matokeo yetu ya utafutaji. Tukijua kuwa watumiaji wanabofya tokeo la kwanza, tunakisia kuwa tunafanya mambo sawa, na kama wanaenda kwa ukurasa unaofuata au weka hoja yao kwa njia mpya, labda tumekosea mahali. Zaidi ya hayo, data ya kumbukumbu hutusaidia kuzuia ulaghai na matumizi mengine mabaya, kama vile hadaa, mashambulizi ya hati na taka, ikiwemo udanganyifu wa mibofyo ya hoja na matangazo.
Tunaweka uwiano unaofaa kati ya shinikizo tunazokabiliana nazo, kama vile faragha ya watumiaji wetu, usalama wa mifumo yetu na hitaji la uvumbuzi. Tunaamini kuwa kuondoa maelezo ya kutambulisha Anwani za IP baada ya miezi 9 na vidakuzi katika kumbukumbu zetu za utafutaji baada ya miezi 18 inaleta hali ya uwiano.
Kama injini tafuti zote, Google ni kioo cha maudhui na maelezo yanayopatikana hadharani kwenye wavuti. Injini tafuti hazina uwezo wa kuondoa maudhui kwenye wavuti moja kwa moja, kwa hivyo kuondoa matokeo ya utafutaji kutoka Google au injini tafuti nyingine huwacha maudhui yaliyopo bila kuathiriwa. Kama unataka kuondoa kitu kwenye wavuti, unafaakuwasiliana na msimamizi wa tovuti hiyo na kuumuliza afanye mabadiliko. Maudhui yakishaondolewa na injini tafuti ya Google imetamba kwenye ukurasa huo tena, maudhui hayo hayatatokea tena katika matokeo ya utafutaji ya Google. Kama una ombi muhimu la kuondoa, unaweza pia kutembelea ukurasa wetu wa msaada kwa maelezo zaidi.
Ndiyo, kama tovuti na injini tafuti nyingi, Google hutumia vidakuzi kuboresha uzoefu wako na kutoa huduma na matangazo. Vidakuzi hutusaidia kuweka rekodi ya mapendeleo yako, kama unataka matokeo yako ya utafutaji yawe kwa kiingereza au Kifaransa, au kama unatumia kichujio chetu cha Utafutaji Salama. Bila vidakuzi Google haingeweza kukumbuka mapendeleo ya watu tofauti. Pia huwa tunatumia vidakuzi kutoa matangazo mwafaka kulingana na mapendeleo yako.
Tumeambiwa kuwa watumiaji wengi hawataki kuweka mipangilio ya kompyuta zao kila wanapoingia. Kama hutaki kupokea vidakuzi unaweza kubadilisha vivinjari vyako kukujulisha vidakuzi vinapotumwa na kisha ukatae vidakuzi kutoka tovuti fulani (au zote). Unaweza pia kufuta vidakuzi kutoka kivinjari chako. Injini tafuti ya Google inaweza kufanya kazi bila vidakuzi, lakini utapoteza baadhi ya vipengee ukichagua kulemaza vidakuzi.
Nchi nyingi hushughulikia maswala ya faragha kwa njia tofauti na hakuna kiwango thabiti ulimwenguni ambacho nchi zote zinakubaliana nacho. Sera ya faragha ya Google imeundwa ili kuwa taarifa moja, wazi na ya kijumla ya mtazamo wetu wa faragha, na desturi zetu za faragha chini yake zimeundwa ili kutekeleza sheria husika duniani.
Kama kampuni zingine za teknologia na mawasiliano, huwa tunapokea maombi kutoka kwa maafisa wa serikali duniani kote kutoa maelezo kuhusu watumiaji wa huduma na bidhaa zetu. Ili kusaidia kuongeza uwazi kuhusu maombi haya tumeunda Zana ya Maombi ya Serikali, ambayo inaonyesha idadi ya maombi ambayo tumepokea yanayohusiana kimsingi na uchunguzi wa uhalifu. Kwa maelezo zaidi kuhusu zana na asili ya maombi haya, tafadhali kagua Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu Zana ya Maombi ya Serikali.
Unaweza kuwasiliana nasi wakati wowote kupitia fomu yetu ya mawasiliano kuhusu faragha. Ukipenda, unaweza pia kuandikia:
Privacy Matters