Tunapatia kulinda faragha kipaumbele kwa kuwa na uwazi kuhusu ni maelezo yapi tunakusanya na jinsi tutakavyotumia maelezo hayo kuonyesha matangazo mwafaka. Pia tunaifanya rahisi kwako kuona, kudhibiti, na kuchagua kujiondoa kwa matangazo yanayokulenga binafsi kwenye huduma kadhaa kutoka tovuti za Google kama vile utafutaji, tovuti za nje za Adsense, na programu za Google. Hakika, hatutauza au kushiriki maelezo yako yanayoweza kukutambulisha kibinafsi yanayotokana na vidakuzi vinavyotoa matangazo kwa wahusika wengine bila ruhusa yako.
Tunatoa matangazo kupitia programu yetu ya Adwords kwenye tovuti zetu pamoja na Mtandao wa Google wa Matangazo ya Maonyesho. Pia tunatoa matangazo kupitia programu zetu za Adsense na Admob kwenye tovuti na huduma za washirika (kama vile programu na teja zingine). Tunatumia mbinu kadhaa kuwasilisha matangazo mwafaka.
KwaMtandao wa Google wa Matangazo ya Maonyesho na mtandao wa AdMob, tunatoa matangazo kulingana na maudhui ya tovuti ambazo umetazama au programu unayotumia kwenye kifaa chako na pia tunaweza kutumia data ya washirika wengine kulenga matangazo. Kwa mfano, ukitembelea tovuti ya kilimo, matangazo kwenye tovuti hiyo yanaweza kuhusiana na kilimo. Kwa kuongezea, tunaweza kutoa matangazo kulingana na unazopenda. Unapovinjari tovuti za Google au tovuti ambazo zimeshirikiana nasi au kupakua na kutumia programu kwenye kifaa chako, Google inaweza kuweka vidakuzi au vitambulishi visivyojulikana (ona zaidi kuhusu vitambulishi visivyojulikana hapa chini) katika kivinjari chako au kwenye kifaa chako ili kuelewa aina ya kurasa zilizotembelewa, maudhui uliyoona au programu kwenye kifaa chako cha mkononi. Kulingana na maelezo haya na/au data isiyo na maelezo ya kutambulisha kutoka kwa washirika wetu, Google huhusisha vidakuzi vyako au vitambulishi visivyojulikana na aina za mambo yanayokuvutia na kutumia aina hizi kuonyesha matangazo kulingana na yanayokuvutia. Kwa mfano, ikiwa wewe hutembelea tovuti za kusafiri mara kwa mara, Google inaweza kuonyesha matangazo zaidi yanayohusiana na usafiri. Au, ukipakua programu ya kandanda, Google inaweza kukuonyesha matangazo yanayohusiana na kandanda. Google inaweza pia kukuonyesha matangazo yanayohusiana na maudhui ya tovuti katika historia yako ya kuvinjari ya hivi karibuni. Google inaweza pia kutumia aina ya kurasa ambazo umetembelea, maudhui ambayo umetazama, au programu kwenye kifaa chako kubashiri demografia kama jinsia yako na umri. Kwa mfano, ikiwa tovuti unazotembelea na programu unazopakua hutembelewa sanasana na wanawake (kulingana na data ya utafiti iliyojumlishwa kuhusu wanaotembelea tovuti au matumizi ya programu), tunaweza kuhusisha vidakuzi vyako na vitambulishi visivyojulikana na demografia ya wanawake.
Zaidi ya matangazo kulingana na unayoyapenda, Google huwaruhusu watangazaji (Google ikiwemo) kukuonyesha matangazo kulingana na maingiliano yako ya awali kwenye wavuti au katika programu, kama vile kutembelea tovuti au programu za watangazaji. Kwa mfano, mtu aliyetembelea tovuti au programu ya ununuzi ya duka la bidhaa za michezo kwenye wavuti anaweza kupokea matangazo kuhusu punguzo maalum kutoka duka hilo.
Google haitahusisha vikundi nyeti vya vivutio na vidakuzi vyako au vitambulishi visivyojulikana (kama vile asili, dini, mwelekeo wa jinsia, afya, au vikundi nyeti vya kifedha), na haitatumia vikundi kama hivi inapokuonyesha matangazo kulingana na unayopenda.
Unapotafuta kitu kwenye Google bila ya kuingia katika Akaunti yako ya Google, ukurasa wa matokeo ya utafutaji huonyesha matokeo na matangazo yanayolingana na maneno yako ya sasa ya utafutaji na eneo lako. Tukionelea kuwa matangazo yatakuwa mwafaka zaidi, tunaweza pia kutumia utafutaji wa hivi karibuni kwa mada zinazohusiana na matangazo uliyobofya ili kuamua ni matangazo yapi tutaonyesha.
Ukiwa umeingia katika Akaunti yako ya Google, tunaweza kutumia maelezo ya ziada kuamua ni matangazo yapi tutaonyesha. Kwa mfano, tunaweza kutumia utafutaji wa hivi karibuni kama tunadhani kuwa utafutaji unahusiana, kwa mfano ukitafuta “Mombasa” kisha utafute “hoteli” -inaweza kuonyesha kwamba unataka kujua kuhusu hoteli mjini Mombasa. Tunatumia utafutaji wa hivi karibuni tu kwa sababu haina maana kuhusisha utafutaji uliofanywa kitambo.
Njia nyingine tunaweza kukuoa matangazo yanayokufaa binafsi kwenye utafutaji ni kwa kutumia Historia yako ya Wavuti kwenye Google. Kwa mfano, kama ulibofya tokeo la utafutaji la tovuti ya vifaa vya kukwea milima, na kisha ukatafuta “likizo”, hii inaweza kuonyesha kwamba unataka mahali pa likizo ambapo unaweza kukwea milima, na huenda ukaona matangazo ya likizo za kukwea milima.
Zaidi ya hayo, tunaweza kutumia maelezo unayotwambia kujihusu ili kulenga matangazo kwenye utafutaji. Kwa mfano, bidhaa zingine zinaweza kukupa nafasi ya kutuambia kwamba unapenda mwuuzaji au kampuni fulani na tunaweza kutumia maelezo hayo baadaye kukuonyesha matangazo ya wafanyabiashara, bidhaa na huduma tunazofikiria unaweza kupenda.
Katika Gmail, matangazo mengi tunayoonyesha hutokea karibu na ujumbe wa barua pepe uliofunguliwa na hulingana na maudhui ya barua pepe yako. Tunapo binafsisha matangazo, tunaonyesha matangazo kulingana na maudhui ya barua pepe zako zote. Kwa mfano, kama hivi karibuni umepokea barua pepe nyingi kuhusu upigaji picha au kamera, tunaweza kukuonyesha punguzo kutoka kwa duka la karibu la kamera.
Sio matangazo yote yanayokulenga binafsi kwenye Utafutaji wa Google, Gmail na tovuti zingine za Google. Tunalenga matangazo kwako binafsi tunapofikiria kuwa maelezo hayo ya ziada yanaboresha matangazo yanayochaguliwa kwako.
Kupitia kidakuzi cha DoubleClick, YouTube pia huonyesha matangazo kulingana na unayopenda ili kuonyesha matangazo mwafaka kwenye tovuti yake. Vikundi vya vivutio huamuliwa na ziara zako kwenye tovuti zinazotumia programu yetu ya AdSense, pamoja na video unazotafuta, unazopendelea kutazama, au hatua unazochukua (kama vile kupakia) kwenye YouTube. Kidakuzi cha DoubleClick huhusisha kivinjari chako na vikundi mwafaka vya vivutio na hutumia vikundi hivi kuonyesha matangazo yanayolingana na unachopenda. Hatuunganishi maelezo ya kibinafsi yanayoweza kukutambulisha kutoka kwa akaunti yako ya YouTube au Akaunti ya Google na data ya Vidakuzi inayotumika kutoa matangazo kulingana na unachopenda bila idhini yako. Ili kujifunza zaidi, tazama Matangazo ya Youtube na Wewe.
Vikundi vya vivutio na demografia huamuliwa na unavyotembelea tovuti katika Mtandao wa Google wa Matangazo ya Onyesho au huduma zingine au programu unazotumia au kupakua. Kupitia Kidhibiti cha Mapendeleo ya Matangazo kwa vivinjari, unaweza kuhariri mapendeleo yako ya matangazo katika vivinjari kwa kuongeza vikundi mwafaka vya mambo yanayokuvutia. Kupitia Kidhibiti cha Mapendeleo ya Matangazo kwa vivinjari na Kidhibiti cha Mapendeleo ya Matangazo kwa programu, unaweza kuondoa vikundi vya vivutio ambavyo havikufai na Google haitavitumia tena kukuonyesha matangazo kulingana na vivutio hivyo. Unaweza pia kubadilisha ni vikundi vipi vya demografia vinahusishwa na vidakuzi vyako au vitambulishi visivyojulikana. Unapo hariri mapendeleo yako ya matangazo, mipangilio yako mipya inaweza kosa kutekelezwa mara moja, kwa sababu inachukuwa muda kwa mabadiliko kuchakatwa katika mifumo yetu.
Kama unapendelea kutopokea matangazo kulingana na mambo yanayokuvutia katika vivinjari vya wavuti, unaweza kubofya kitufe cha “Chagua kujiondoa” kwenye Kidhibiti cha Mapendeleo ya Matangazo. Unapofikia wavuti kupitia kivinjari, Google hutoa chaguo kadhaa za kuhifadhi kabisa mipangilio yako ya kuchagua kujiondoa katika kivinjari chako. Baada ya kuchagua kujiondoa, Google haitakusanya maelezo ya vikundi vya vivutio na hutapokea matangazo kulingana na mambo yanayokuvutia kupitia Google unapofikia wavuti kupitia kivinjari. Bado utaona idadi sawa ya matangazo kama awali, na Google bado inaweza kukuonyesha matangazo mwafaka kulingana na maudhui ya ukurasa wa wavuti au maelezo mengine yasiyo ya kibinafsi. Kwa mfano, ukitembelea tovuti ya kilimo, Google inaweza kuamua maudhui ya wavuti na inaweza kuonyesha matangazo kiotomatiki yanayohusiana na kilimo cha bustani kwa wageni wote bila kutumia kidakuzi. Zaidi ya hayo, kila mara tunapotoa tangazo kwenye utafutaji wa Google au kwenye tovuti za AdSense kwa washirika wa utafutaji, matangazo yanayoonyeshwa yanaweza bado kulingana na maneno ya utafutaji unayoingiza.
Kama unapendelea usipokee matangazo kulingana na mambo yanayokuvutia katika programu zinazotumia vitambulishi visivyojulikana, unaweza kuchagua kujiondoa kwa kutumia kidhibti chaa mapendeleo kinachofaa.
Kidhibiti cha Mapendeleo ya Matangazo ni tovuti ya Google ambapo unaweza kudhibiti mipangilio inayohusiana na matangazo unayoona. Lengo letu ni kukupa uwazi na chaguo kuhusu matangazo tunayokuonyesha.
Kidakuzi ni kijisehemu cha maandishi kinachotumwa kutoka seva ya tovuti na kuhifadhiwa kwenye kivinjari cha wavuti. Kama tovuti na injini tafuti nyingi, Google hutumia vidakuzi ili kutoa uzoefu bora kwa watumiaji na kutoa matangazo mwafaka.
Google hutumia kidakuzi cha DoubleClick kwenye tovuti za AdSense, tovuti za washirika na baadhi ya huduma za Google ili kutoa matangazo mwafaka zaidi kwenye wavuti na kupunguza mara unazoona tangazo fulani. Unapotembelea tovuti, kutazama au kubofya tangazo linaloauniwa na huduma za utangazaji za Google, tunaweza kuweka kidakuzi kwenye kivinjari chako. Kidakuzi hiki cha utangazaji kitaonekana katika kivinjari chako kama kinatoka kutoka kwa kikoa “doubleclik.net.”
Kidakuzi kinapowekwa katika kivinjari chako, kinaruhusu Google kukusanya maelezo kuhusu maingiliano ya kivinjari chako na tangazo fulani. Maelezo yanarekodiwa katika kumbukumbu ambayo inafanana hivi:
time: 06/Aug/2008 12:01:32
ad_placement_id: 105
ad_id: 1003
userid: 0000000000000001
client_ip: 123.45.67.89
referral_url: "http://youtube.com/categories"
Sehemu ya “wakati” huonyesha wakati tangazo lilionyeshwa. “kitambulishi cha kuweka tangazo” na “kitambulishi cha tangazo” hutambua kampeni ya utangazaji na tangazo maalum lililotolewa. “userrid” ni kidakuzi cha tangazo la onyesho kinachotambulisha kivinjari. “IP ya teja” huonyesha awwani ya IP ya mtumiaji. “URL ya kurejelea” inaonyesha URL ya ukurasa ambapo tangazo lilitolewa. Kumbukumbu zetu pia hurekodi kama kivinjari cha mtumiaji hubofya au kuingiana na tangazo.
Maelezo haya husaidia Google kuwasilisha matangazo mwafaka kulingana na mambo yanayokuvutia, kudhibiti utaona tangazo fulani mara ngapi, na kupima utendakazi wa kampeni za matangazo. Yeyote anayependelea kutoona matangazo mwafaka kwa kiwango hiki anaweza kuchagua kujiondoa. Kuchagua kujiondoa kutakuwa mahsusi kwa kivinjari unachotumia pekee ukibofya kitufe cha “Chagua kujiondoa”.
Kutoa matangazo katika huduma ambazo teknologia ya kidakuzi inaweza kuwa haipatikani (kwa mfano, katika programu na wateja wengine), tunaweza kutumiavitambulishi visivyojulikana. Kutoa matangazo mwafaka na yanayolenga mambo yanayokuvutia, tunaweza kutumia maelezo kuhusu shughuli zako katika huduma hizi, pamoja na maelezo yasiyo yasiyokutambulisha kibinasfsi, kama vile data ya demografia.
Huenda programu za vifaa vya mkononi zikaweza kufikia kitambulishi cha kifaa chako na huenda zikaipitisha kwa Google wakati unapotumia programu ambayo huonyesha matangazo ya Google AdSense au AdMob. Iwe tumepokea kitambulishi cha kifaa chako au la, tunahusisha tu maelezo ya moja kwa moja yenye vitambulishi visivyo na jina, sio na vitambulishi vya vifaa vyenyewe. Katika kesi ambazo tunapokea kitambulishi chako cha kifaa, kitambulishi kisichokuwa na jina kitaundwa kwa ushirikiano na kifaa chako. Hii hukuwezesha kuwa na udhibiti kamili, kwa sababu tofauti na kitambulishi kifaa ambacho huwezi kukibadilisha au kukifuta, unaweza kuchagua kuweka upya au kulemaza vitambulishi visivyo na jina wakati wowote.
Google Analytics ni zana ya uchanganuzi ya wavuti inayotolewa na Google bila malipo inayosaidia wanaomiliki tovuti kuelewa jinsi wageni wanavyoingiliana na tovuti yao. Google Analytics hukusanya maelezo bila kujulikana, na sana kama kukagua wayo katika mchanga, huripoti mitindo ya wavuti bila ya kutambulisha wageni binafsi. Analytics hutumia vidakuzi vyake yenyewe ili kufuata maingiliano ya wageni. Vidakuzi hivi hutumiwa kuhifadhi maelezo, kama vile ni saa ngapi tovuti ilitembelewa, kama mgeni ametembelea tovuti hiyo tena, na ni tovuti ipi ilimwelekeza mgeni kwa ukurasa huo wa wavuti. Wateja wa Google Analytics wanaweza kuona ripoti mbalimbali kuhusu jinsi wageni wanaingiliana na tovuti yao ili waboreshe tovuti yao na jinsi watu wanavyoipata. Seti tofauti ya vidakuzi hutumika kwa kila tovuti, na wageni hawafwatwi katika tovuti nyingi. Wateja wa Analytics wanawajibishwa kuwajulisha watumiaji kuhusu matumizi yao wa programu ya uchanganuzi. Kulemaza aina hii ya kidakuzi, vivinjari vingine vitaonyesha wakati kidakuzi kinatumwa na kukuruhusu kukataa vidakuzi kimoja kimoja. Zaidi ya kukataa vidakuzi, unaweza pia kusakinisha Programu Jalizi ya Kujiondoa kwenye Google Analytics katika kivinjari chako, ambayo inazuia Google Analytics isikukusanye maelezo kuhusu matembezi yako kwenye tovuti mbalimbali.
Zaidi ya vidakuzi vya Google Analytics na DoubleClick, Google hutumia vidakuzi kusaidia biashara zinazonunua matangazo kutoka Google kuamua ni watu wangapi kati ya wale wanaobofya matangazo yao wanunua bidhaa zao mwishowe. Kidakuzi cha kufuata kushawishika huwekwa kwenye kivinjari chako unapobofya tangazo linalowasilishwa na Google mahali mtangaziji amechagua kufuatilia kushawishika tu. Vidakuzi hivi humalizika baada ya siku 30 na havina maelezo yanayoweza kukutambulisha kibinafsi. Kama kidakuzi hiki bado hakijapitwa na wakati unapotembelea kurasa zingine za tovuti ya mtangazaji, Google na mtangazaji wataweza kujua kuwa ulibofya tangazo na ukaendelea kwa ukurasa huo. Kila mtangazaji hupata kidakuzi tofauti, kwa hivyo hakuna kidakuzi kinachoweza kufuatwa katika tovuti zote za mtangazaji. Kama unataka kulemaza vidakuzi vya kufuata kushawishika, unaweza kuweka kivinjari chako kizuie vidakuzi kutoka kwa kikoa cha googleadservices.com.
Zaidi ya hayo, kwa sababu hakuna mipangilio ya kidakuzi kwa kila kikoa katika iOS na vivinjari vya simu ya mkononi vya Android, lazima ulemaze vidakuzi vyote ili kuchagua kutoka kwa kufuata mazungumzo ya simu ya mkononi.
Unaweza kutumia Meneja ya Mapendeleo ya Matangazo ya programu ili kuhariri kategoria husika za maslahi, kuweka upya mapendeleo yako ya matangazo, au kutoka kwa matangazo yanayotegemea maslahi kwenye kifaa chako cha mkononi.
Ili kubadilisha mapendeleo yako, fuata maagizo hapa chini ya kifaa chako cha mkononi.
Android
iOS
Huenda mapendeleo yako ya matangazo ya programu za kifaa cha mkononi yakatekelezwa pia kwenye “Matangazo kutoka Google” katika kivinjari chako cha wavuti na kinyume chake. Ili kudhibiti mapendeleo yako ya matangazo ya “Matangazo kutoka Google” unayoyaona katika vivinjari, tembelea Meneja ya Mapendeleo ya Matangazo ya vivinjari.