Maswali Yanayoulizwa Sana
Google hulinda aje ufaragha wangu na kuweka maelezo yangu salama?
Tunajua usalama na faragha ni muhimu kwako - na ni muhimu kwetu, pia. Tunaifanya kipaumbele kukupa usalama dhabiti na kukupa imani ya kwamba maelezo yako ni salama na kupatikana unapoyahitaji.
Daima tunafanya kazi ili kuhakikisha usalama dhabiti, kulinda ufaragha wako, na kufanya Google ya kufaa zaidi na fanisi kwako. Tunatumia mamia ya mamilioni ya dola kila mwaka na usalama, na kuajiri wataalamu maarufu duniani katika usalama wa data ili kuweka maelezo yako salama. Pia tuliunda zana rahisi kutumia za ufaragha na usalama kama vile Dashibodi ya Google,Uthibitishaji wa hatua -2 na Kidhibiti cha Mapendeleo ya Matangazo. Kwa hivyo ikija kwa maelezo unayoshiriki na Google, utakuwa dhibiti.
Unaweza kujifunza zaidi kuhusu usalama na usalama mtandaoni, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kujilinda na familia yako mtandaoni kwenye tovuti yetu ya Vyema Kujua.
Nawezaje kuondoa maelezo kunihusu kwenye matokeo ya utafutaji ya Google?
Matokeo ya utafutaji Google ni mfano wa maudhui yanayopatikana na umma kwenye wavuti. Injini tafuti haiwezi kuondoa maudhui moja kwa moja kutoka kwa tovuti, kwa hivyo kuondoa matokeo ya utafutaji kutoka Google hakuwezi kuondoa maudhui kutoka kwa tovuti. Ikiwa unataka kuondoa kitu kutoka kwa wavuti, unafaa kuwasiliana na msimamizi wa wavuti wa tovuti ambayo maelezo yamechapishwa na kumuliza afanye mabadiliko. Mara maudhui yakiondolewa na Google imeona usasishaji, maelezo hayatapatikana katika matokeo ya utafutaji ya Google. Kama una ombi muhimu la kuondoa, unaweza pia kutembelea ukurasa wetu wa msaada kwa maelezo zaidi.
Nawezaje kuwasiliana na Google kama nina swali au malalamiko kuhusu faragha?
Unaweza kuwasiliana nasi wakati wowote kupitia fomu yetu yamawasiliano kuhusu faragha.
