Tumejitolea kuboresha usalama wako, kulinda ufaragha wako, na kuunda zana rahisi ili kukupa chaguo na udhibiti.

Vyema Kujua

Tunalenga kukupa zana dhabiti zaidi duniani za usalama na faragha. Usalama na faragha ni muhimu kwetu, tunajua jinsi ilivyo muhimu kwako na tunafanya bidii kuzifanya sawa. Tovuti yetu ya Vyema Kujua hukusaidia na familia yako kuwa salama mtandaoni. Itembele ili kupata maelezo zaidi na kuelewa jinsi Google husaidia kukuweka salama, kompyuta yako na Wavuti kutoka kwa uhalifu wa saibe.

Kuwa salama mtandaoni

Tunaendelea kufanya kazi ili kuhakikisha usalama dhabiti, kulinda ufaragha wako, na kufanya Google ya manufaa zaidi na fanisi kwako. Tunakupa zana na vidhibiti ili kuamua ni nini unashiriki, na nani na jinsi gani-na tunaifanya salama na bila ya kusumbua.

Uthibitishaji wa hatua -2

Uthibitishaji wa hatua -2 hufanya akaunti yako ya Google salama kwa kuilinda na kitu unachokijua (nenosiri lako) na kitu ulichonacho (simu yako). Jua jinsi ya kusanidi Uthibitishaji wa hatua -2.

Modi chini kwa chini

Katika modi chini kwa chini, kurasa unazofungua na faili unazopakua hazirekodiwi katika historia ya kuvinjari au kupakua ya Chrome. Fahamu jinsi ya kufikia modi chini kwa chini.