Kuingia na kuondoka
Kuingia kwenye akaunti yako ya Google ni rahisi – bofya tu kwenye kitufe cha Ingia kwenye upande wa juu wa huduma yoyote ya Google kuangalia Gmail yako, kupakia video kwenye YouTube au kupata tu matokeo ya utafutaji yanayohusiana zaidi.
Lakini unapokuwa ukitumia kompyuta za hadhira kama kwenye mkahawabwake au maktaba, kumbuka kuwa unaweza ukawa bado umeingia katika huduma zozote ulizokuwa ukitumia hata baada ya kufunga kivinjari. Hivyo unapokuwa ukitumia kompyuta ya hadhira, hakikisha umetoka kwa kubofya kwenye picha yako ya akaunti au anwani ya barua pepe kwenye upande wa juu wa mkono wa kulia na kuchagua Ondoka.
Ukitumia kompyuta za hadhara mara kwa mara, tumia uthibitishaji wa hatua 2 ili kusaidia kuweka akaunti yako salama, na kuwa mwangalifu sana kutoka kwenye akaunti zako na kuzima kivinjari chako unapokuwa umemaliza kutumia wavuti.
