Tumia mitandao salama

Ni vizuri kuwa makini zaidi unapoingia mtandaoni ukitumia mtandao usioufahamu au kuamini – kama kutumia mtandao wa Wi-Fi wa bila malipo katika mkahawabwake wa karibu nawe. Mtoa huduma anaweza kuchungua trafiki yote kwenye mitandao yao, ambako kunaweza kujumuisha maelezo yako.

Hata hivyo, ikiwa unatumia huduma inayosimba kwa njia fiche muunganisho wako kwenda kwenye huduma ya wavuti, inaweza kuifanya vigumu zaidi kwa mtu kuchungulia shughuli zako. Kwa chaguo-msingi, tunaweka usimbaji fiche kwa muunganisho wa Gmail kati ya kompyuta yako na Google – hii husaidia kulinda shughuli zako za Google kutokana na kuchunguliwa na wengine. Pia tunafanya muunganisho huu, unaojulikana kama kipindi kipana Usimbaji fiche wa SSL , kuwa chaguo-msingi unapoingia kwenye Hifadhi ya Google na huduma nyingine nyingi.

Angalia ishara kuhusu muunganisho wako ulio na tovuti unapovinjari mtandaoni.

Kwanza, angalia upau anwani kwenye kivinjari chako uone kama URL ni halisi. Unapaswa pia kuangalia uone kama anwani ya wavuti inaanza na https:// – inayoashiria kuwa muunganisho wako wa tovuti umesimbwa kwa njia fiche na ni sugu zaidi kwa kuchungulia au kuchezea. Baadhi ya vivinjari pia hujumuisha ikoni ya kufuli katika upau anwani kando yaa https:// kuonyesha wazi kuwa muunganisho wako umesimbwa kwa njia fiche na umeuganishwa kwa usalama zaidi.

Unapounganishwa kupitia mtandao wa Wi-Fi wa hadhara, yeyote katika maeneo ya jirani anaweza kufuatilia maelezo yanayopita kati ya kompyuta yako na mtandao-hewa wa Wi-Fi ikiwa muunganisho wako haujasimbwa kwa njia fiche. Epuka kufanya shughuli muhimu kama benki au ununuzi kupitia mitandao ya hadhara.

Ikiwa unatumia Wi-Fi nyumbani, unapaswa kuhakikisha kuwa unatumia nenosiri kuweka salama ruta yako. Fuata tu maagizo yaliyotolewa na Mtoa Huduma wako wa Intaneti au mtengenezaji wa ruta ili uweke nenosiri lako binafsi kwenye ruta badala ya kutumia nenosiri chaguomsingi la ruta, ambalo linajulikana kwa wahalifu. Ikiwa wahalifu wataweza kufikia ruta yako, wanaweza kubadilisha mipangilio yako na kuchungulia shughuli zako mtandaoni.

Hatimaye, unapaswa kuhakikisha kuwa unauweka salama mtandao wako wa nyumbani wa Wi-Fi ili watu wengine wasiweze kuutumia kwa ajili ya safu ya ziada ya usalama. Hii inamaanisha kuweka nenosiri la kulinda mtandao wako wa Wi-Fi – na kama tu manenosiri mengine unayochagua, hakikisha unachagua refu, mchanganyiko wa kipekee wa nambari, herufi na alama ili wengine wasiweze kukisia kwa urahisi nenosiri lako. Unapaswa kuchagua mpangilio wa WPA2 unaposanidi mtandao wako kwa ajili ya usalama mahiri.