Jinsi ya kulinda familia yako kwenye intaneti

Tunafahamu umuhimu wa kuwalinda na kuwaelimisha vijana juu ya kutumia intaneti na tunataka kuwapa watumiaji wetu wote hali salama.

Kuhusiana na usalama wa familia, lengo letu ni:

  • Kuwapa wazazi na walimu nyenzo za kuwasaidia kuchagua maudhui ambayo watoto wao wataona kwenye intaneti
  • Kutoa vidokezo na ushauri kwa familia kuhusu jinsi ya kuwa salama kwenye intaneti
  • Kushirikiana kwa karibu na mashirika kama vile ya ufadhili, kampuni zingine katika sekta yetu na mashirika ya serikali yanayoshughulika na kuwalinda vijana

Tazama video zaidi kuhusu usalama kwenye kituo chetu cha YouTube

Zana za usalama kutoka Google

Jifahamishe kuhusu nyenzo mpya zaidi ambazo Google hutoa kwa wazazi na walezi.

Kuripoti maudhui yasiyofaa

Fahamu jinsi ya kutuarifu ukipata maudhui ambayo hayapaswi kuwa kwenye tovuti kama vile Google+, YouTube na Blogger.

Vidhibiti vya kushiriki na mipangilio ya faragha

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kudhibiti maudhui unayoshiriki kwenye intaneti - zikiwemo picha, blogu za kibinafsi na maelezo ya wasifu.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Ikiwa una swali kuhusu Google na usalama wa watoto, unaweza kupata jibu lako katika ukurasa wa maswali yanayoulizwa sana.